Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na wizara ya mambo ya ndani nchini Saudi Arabia ni kwamba zaidi ya wasaudi Arabia 2000 wamejiunga na vikundi vya kigaidi na wako katika nchi za jirani wanapingana upande wa magaidi ikiwemo nchi ya Syria, Iraq na Yemen.
Aidha msemaji wa wizara hiyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Gazeti la “AL-Hyat” nakusisistiza kuwa: wananchi 2093 wa Saudi Arabia wako nje ya nchi wamejiunga na vikundi vya kigaid, ambapo 1540 kati yao wako katika safu za magaidi nchini Syria dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
“Mansur Turkiy” aendlea kusema kuwa wananchi 147 kati yao wamejiunga na kikundi cha kigaidi cha Alqaida na hivi sasa wako nchini Yemen wakipambana dhidi ya serikali ya nchi hiyo, pia amesema wananchi watano katika magaidi hao wako nchini Iraq wakishirikiana na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Aidha amemalizia kwa kusema kuwa: wananchi 31 kati ya magaidi hao wako nchini Pakistan na Afghanistan, huku akisisitoza kuwa wananchi 73 wa Saudi Arabia wamefungwa katika nchi mbaimbali duniani kwa tuhuma ya kuhusika na vitendo vya kigaidi katika mataifa hayo.
Wengi miungoni mwa wahariri wanaamini kuwa: pamoja yakuwa wizara hiyo imetoa takwimu hiyo inayoonyesha idadi ya kuwepo kwa magaidi wengi kutoka taifa hilo, ama wanadai kuwa ukwili unaonyesha kuwa kunazaidi ya idadi iliokuwa imetajwa na wizara hiyo, hasa ukizingatia kwamba ripoti ya wizara hiyo haijaashiria takwimu ya magaidi waliokufa wakiwa katika safu za magaidi hao.
mwisho/290
27 Desemba 2016 - 19:27
Msimbo wa Habari: 801193
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imetangaza kuwa wananchi wake 2000 wamejiunga na vikundi vya kigaid, ambapo wako katika nchi jirani za mashariki ya kati ikiwemo Syria, Iraq, Yemen wakiwa pamoja na vikundi vya kigaidi nakukabiliana na serikali za nchi hizo